WAJUE HIP HOP CASH KINGS 2017
Siku chache zilizopita jarida la forbes limetoa listi ya wanamuziki wa hiphop wenye mkwanja mrefu kwa sasa duniani.
Katika listi hiyo kuna baadhi ya mastaa wamezidi kupanda na baadhi wameweza kushuka kwa namna moja ama nyingine.
Ifuatayo ni tano bora ya wasanii wa hip hop wenye mkwanja mrefu kwa sasa.
1. P.Diddy (Dirty Money)
Ameendelea kushikilia rekodi yakuwa mwanahiphop mwenye mkwanja mrefu kwa sasa duniani baada yakufanya vizuri kwa mwaka jana. Diddy anamilika makampuni mbali mbali nje ya muziki kama kampuni yakutengeneza Ciroc vodka na lebo ya bad boys entertainment, ambapo kwa mwaka jana waliweza kufanya tour yakimuziki iliyofahamika kama bad boys tour. Ana utajiri wa dola milioni 820.
2. Jay-Z
Ameweza kupanda hadi nafasi ya pili kwa mwaka huu toka mwaka 2014, akiweza kumshusha prodyuza Dr.Dre kwa mara ya kwanza. Hii Imetokana na mafanikio mazuri yakibiashara na uwekezaji alioufanya kwa mwaka jana ambapo aliweza kupata faida ya zaidi ya 30% na mauzo ya zaidi ya dola milioni 200 kupitia platform yake yakuuzia muziki mtandaoni ufahamikao kama tidal. Anamiliki brandi ya shampeni ittwayo, Armac de brignac pamoja na lebo ya muziki ifahamikayo kama Roc Nation. Ana utajiri wa dola milioni 810
3. Dr.Dre
Ameweza kushuka toka nafasi ya pili hadi ya tatu kwa mwaka 2017. Mwaka jana haukuwa mwaka mzuri kibiashara kwa upande wake ila hii haijamfanya asiweze kuingia katika tano bora. Ameweza kuweka rekodi ya mauzo kupitia kampuni yake ya beats by Dre alipoiuza kwa facebook mwaka 2014 nakuweza kuwa Multi Milionea ndani ya siku moja. Alinunua jumba la kifahari huko los Angeles lenye thamani ya dola milioni 40 ambapo kwa sasa thamani hiyo imeongezeka kwa zaidi ya asilimia 20. Utajiri wake una thamani ya dola milioni 740 licha ya yeye Dre kujitangaza mwanamuziki bilionea hapo kabla.
4. Birdman
Ni mmiliki wa lebo ya Cash Money records yenye mastaa kama Drake, Nicki Minaj na Lil wayne ambapo tetesi zinasema wako katika hatua zakuachana na lebo hiyo. Birdman amweza kushika nafasi ya nne katika listi hii kwa mkwanja mrefu. Jina lake halisi ni Bryan Williams, katika listi hii imeonekana kuna utofauti mkubwakati ya tatu bora na nafasi ya nne na ya tano kutokana na thamani ya utajiri wa namba tatu za juu na nafasi ya nne. Birdman ana utajiri wa dola milioni 110 tu, utofauti wa zaidi ya dola milioni 630 na Dr.Dre anayeshika nafasi ya tatu.
5. Drake
Ni msanii ndani ya lebo ya cash money lakini hii haimzuii kutengenea mkwanja mrefu kupitia mziki wake. Drake ambaye jina lake halisi ni Aubrey Graham ameweza kuvuta mkwaja mrefu mwaka huu. Mwaka jana katika Apple music albamu yake imeweza kuangaliwa zaidi ya bilioni moja na kuweka rekodi ya kuwa mwanamuziki wa kwanza katika stoo hiyo kufanya hivyo. Mikataba yakibiashara na nike, sprite na kampuni ya Apple imeweza kumfanya kufunga tano bora hii kwa mkwanja mrefu. Tour yake ya From Atlanta to amsterdam imeweza pia kumuingizia pesa nyingi ambapo tozo ya show moja ilikuwa ni dola milioni moja za kimarekani. Anautajiri wa dola milioni 90.
No comments