HATIMAYE RUNGU LAKUAMUA BINGWA WA EPL AKABIDHIWA CHELSEA
Klabu ya soka nchini Uingereza Tottenham Hotspurs jana usiku ilipata pigo katika mbio zake zakuwania ubingwa wa epl baada yakukubali kichapo kutoka kwa wagonga nyundo wa jiji la London West Ham United ktk mwendelezo wa mechi za ligi kuu nchini humo.
Katika mchezo huo West Ham iliizamisha klabu ya Tottenham kwa kichapo cha goli moja kwa bila katika uwanja wa London stadium. West ham waliokuwa nyumbani walijipatia goli hilo dakika ya 65" kupitia mshambuliaji wao Lanzini baada yakupokea pasi nzuri kutoka kwa Andre Ayew.
Ushindi huo wa jana unaiweka klabu ya Chelsea katika nafasi nzuri yakubeba taji hilo msimu huu.
No comments