HATIMAYE MANCHESTER UNITED YATUA STOCKHOLM
Jana ulikuwa usiku wa "EUROPA LEAGUE" barani ulaya ambapo kulikuwa na ngwe ya pili ya nusu fainali ya michuano hiyo. Klabu ya soka nchini Uingereza Machester United ilikuwa nyumbani old trafford kuikaribisha klabu ya Celta vigo kutoka nchini Hispania katika mchezo wa marudiano wa michuano hiyo.
Ikumbukwe katika mchezo wa kwanza wa ligi hiyo Manchester United waliweza kuibuka na ushindi wa goli moja kwa bila, goli likifungwa na Marcus Rashford.
Usiku wa jana ulikuwa wa furaha na burudani kwa mashabiki wa klabu hiyo baada ya klabu yao kuweza kuingia fainali ya michuano hiyo kwa mara ya kwanza toka ilipobadilishwa jina kutoka" Uefa Cup" nakuitwa "Europa League".
Katika mchezo huo Manchester United iliweza kutoka suluhu ya magoli 1-1 na celta vigo nakuweza kupata ushindi wa jumla wa magoli mawili kwa moja kwa mechi zote mbili. Manchester United ilikuwa ya kwanza kupata goli kupitia kwa Maroune fellaini katika dakika ya 17' kabla ya Celta Vigo kusawazisha goli hilo katika dakika ya 85' kupitia kwa mchezaji wao Roncaglia. Pia katika mtanange beki wa manchester United Eric Bailly na mfungaji wa goli la kusawazisha Roncaglia waliweza kuonyeshwa kadi nyekundu nakutolewa nje ya mchezo baada yakufanyiana madhambi.
Hii itakuwa mara ya kwanza kwa kocha wa Manchester United Jose Mourinho kuingia fainali hizi, na pia nafasi nzuri kwake kuweza kubeba kombe hili kwa mara ya kwanza.
Fainali hizi itaikutanisha klabu ya Manchester United dhidi ya Ajax kutoka nchini Uholanzi katika jiji la Stockholm hapo baadae mei 24.
No comments