UTATA WA KAULI WAIBUKA KATIKA MKUTANO WA RAIS PUTIN NA RAIS MACRON
Ikiwa ni masaa machache tangu Raisi wa Urusi Vladmir Putin alipokutana na Raisi mpya wa Ufaransa Emanuel Macron, yameibua maswali mengi kwa wanadiplomasia na watu mbali mbali duniani.
Licha ya Maraisi hao kukutana na kufanya mkutano wao wa kwanza tangu kuchaguliwa kwa Raisi mpya wa Ufaransa, kauli tata zaibuka katika mkutano huo.
Mengi yalijadiliwa ila kikubwa ni Kipaumbele cha Raisi wa Ufaransa Kuhimiza ushirikiano na kufufua mahusiano na Urusi juu ya kuudhibiti ugaidi nchini Syria. Hali imekuwa tofauti kwa mshiriki wake baada ya Raisi Putin kudai ni wakati muafaka kwa nchi yake kufufua ushirikiano mpya wakibiashara na Uchumi baada ya vikwazo vya muda mrefu kwa nchi hizo mbili.
Mkutano huo uliofanyika katika jiji la Versailles nchini Ufaransa umeibua mirengo mipya kwa maraisi hao wawili licha ya Raisi macron kudai mkutano ulikuwa wa utulivu, tija na matunda mazuri kwa nchi hizo mbili.
30-05-2017; AFRISTEPHO BLOG
No comments