MAPYA YAIBUKA JUU YA "WANNACRY RANSOMWARE"


Watafiti na wataalamu wa mitandao wameibua mjadala na ushahidi mwingine juu ya kirusi hatari cha kompyuta kinachofahamika kama "wannacry". Watafiti hao wamegundua lugha na mipangilio ya kirusi hicho kinashahabiana na muundo wa maneno na lugha ya kichina.
Watafiti hao wameenda mbali zaidi nakudai kirusi hicho kina uhusiano na wadukuzi wakimtandao wakichina. Kinachostaajabisha zaidi ni kuwa kirusi hicho kinaweza kunyumbuliwa kwa lugha 28 tu  ila katika lugha zote hizo ni lugha mbili tu zinaonekana zimeandikwa na mwanadamu ambayo ni lugha ya 'kiingereza' na 'kichina' huku zingine zikiwa hazijaandikwa na mwanadamu.
Mpaka  sasa kirusi hiki kimeshambulia kompyuta takribani laki mbili duniani kwa taasisi za serikali na zisizo za kiserikali pamoja na makampuni binafsi na ya afya pia. Watafiti bado wanaendelea kupata ufumbuzi juu ya kirusi hiki.

30-05-2017; AFRISTEPHO BLOG




No comments

Powered by Blogger.
"