HATIMAYE KOCHA ARSENE WENGER AKUTANA NA MMILIKI WA ARSENAL STAN KROENKE
Jumatatu ya jana ilikuwa ya kitofauti kwa kocha wa Arsenal, Arsene Wenger baada ya kukutana na mmiliki wa klabu hiyo na tajiri wakimarekani Stan Kroenke. Katika mkutano huo mengi yamejadiliwa lakini kikubwa ilikuwa juu ya hatma ya kocha Arsene Wenger ndani ya klabu hiyo.
Hii imechagizwa na muda uliobaki ndani ya mkataba wake wa sasa na klabu hiyo pamoja na kelele na presha za mashabiki wanaotaka mabadiliko ndani ya klabu hiyo kwa sasa. Licha yakushinda taji la Saba la kombe la FA kama kocha wa klabu hiyo, bado ana upinzani mkali kutoka kwa mashabiki wa klabu hiyo wanaomtaka aondoke.
Katika siku hiyo ya jana kocha Arsene wenger alipata pia kukutana na mwenyekiti wa klabu hiyo Ivan Gazidis na kujadili mambo kadhaa wa kadha lakini alitumia muda mwingi kuongea na mmiliki wa klabu hiyo.
Ikumbukwe mmiliki wa klabu hiyo amewahi kukiri kwa nyakati tofauti kuwa yuko tayari kumsapoti kocha huyo ili kuweza kubeba taji la ligi kwa msimu ujao.
Arsenal waliweza kufungwa mechi 7 ndani ya mechi 12 kati ya Januari 31 na Aprili 10, ikiwemo kipigo cha goli 10-2 toka kwa Bayern Munchen.
Tayari kocha Arsene Wenger amewekewa mkataba mpya mezani na klabu hiyo toka miezi michache iliyopita ila bado kocha huyo hajaamua hatma yake ndani ya klabu hiyo.
Wakati huo huo kocha Arsene Wenger ameshauri bodi ifanye maamuzi kwa uhalisia kuliko kusikiliza kwa kelele na misukumo ya mashabiki wa klabu hiyo.
30-05-2017; AFRISTEPHO BLOG
No comments