FRANCESCO TOTTI AONDOKA NA KOCHA NDANI YA AS ROMA
Ni siku chache tangu mmoja wa wachezaji mashuhuri wa klabu ya As Roma Francesco Totti kutundika daluga kutumikia klabu hiyo, hatimaye klabu hiyo imemuachisha kazi kocha wake Lucciano Spalletti baada ya kudumu nae kwa miezi 16 tangu alipotua klabuni hapo.
"tunapenda kumshukuru Spalletti kwa ufanyaji wake wa kazi na juhudi zake ndani ya klabu, muda wake apa ndani ya klabu umeweza kuifanya Roma kushinda pointi nyingi na magoli mengine katika historia ya klabu hiyo, na pia tunamtakia mafanikio mema huko aendako" alisema Raisi wa klabu hiyo Jim Pallotta
Spalletti mwenye umri wa miaka 58, aliweza kuingoza Roma kushinda mataji mawili ya Coppa Italia kati ya mwaka 2005-2009 kabla yakutimua zake nchini Urusi katika klabu ya Zenit St. Petersburg.
Tetesi zinasema huenda kocha huyu akajiunga na Inter Milan.
30-05-2017; AFRISTEPHO BLOG
No comments