MFAHAMU KOCHA MPYA WA BARCELONA


Ikiwa ni masaa kadhaa yamepita tangu klabu ya Barcelona kumtangaza kocha Ernesto Valverde kuwa mrithi mpya wa kocha Luis Enrique alietangaza kuachia ngazi tangu mwezi Machi mwaka huu. valverde anachukua mikoba ya Luis Enrique akitokea klabu ya Athletic Bilbao ya nchini humo.
Ernesto Valverde amepewa Kandarasi ya miaka miwili ndani ya klabu hiyo na mmoja wa nyongeza kulingana na jinsi atakavyoiongoza klabu hiyo. Kuteuliwa kwa kocha Valverde kuiongoza barcelona kunamaliza muda wa miaka minne aliyokuwa anaiongoza klabu ya Athletic Bilbao kama kocha mkuu.
Hii inahitimisha utawala wa Luis Enrique ndani ya klabu hiyo ambapo aliweza kushinda mataji matatu (treble trophies) katika msimu wake wa kwanza klabuni hapo.
Valverde ambaye aliwahi kuichezea Barcelona kama mshambuliaji, anarudi tena klabuni hapo kama kocha mkuu.
Raisi wa klabu ya Barcelona Josep Maria Bartomeu amesifia uwezo wa kocha huyu mwenye umri wa miaka 53 kwa kusema ni mzoefu, mwenye akili na busara, mbunifu na zaidi anacheza mfumo na staili ya Barcelona  kwa kuwapandisha vijana kutoka ngazi ya chini hadi kucheza timu kubwa.
Ernesto Valverde ni mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Hispania pamoja na Barcelona. Amezaliwa Februari 9 mwaka 1964 katika mji wa "viandar De La vera" nchini Hispania, na sasa ana umri wa miaka 53. Amewahi kuzichezea klabu za Barcelona (michezo 22 nakufunga magoli 8 kati ya mwaka 1988-1990), Athletic Bilbao (1990-1996 michezo 170 nakufunga magoli 44), pamoja na klabu zingine kama Sestao, Alaves, Espanyol na Mallorca.
Aliweza pia kuchezea timu ya taifa kwa ngazi tofauti na Timu ya taifa ngazi kuu mechi moja tu. Katika ngazi ya ukocha ameweza kuzifundisha klabu mbali mbali kwa nyakati tofauti kama Athletic bilbao, Villareal, Olympiacos, Espanyol na sasa klabu ya Barcelona.



30-05-2017; AFRISTEPHO BLOG, copyright@2017




No comments

Powered by Blogger.
"