MAREKANI YAZIDI KUJIIMARISHA


Wakati hofu na sintofahamu juu ya hatma ya mzozo wa Marekani na Korea kaskazini  ikiendelea, jeshi la Marekani lazidi jiimarisha na kuboresha miundombinu yake yakijeshi.
Kwa mara ya kwanza jeshi la Marekani wamefanikiwa jaribio lao la kivita juu ya mitambo yakuzuia mabomu yanayofahamika kama "Inter continental ballistic missile". Wamefanikiwa kujaribu mitambo yakuzuia mabomu hayo na matokeo yamekuwa mazuri kwa nchi hiyo.
Pentagon walitoa taarifa juu ya jaribio hili nakudai kuwa mpango huu wa majaribio ulikuwa wa muda mrefu lakini umefanyika sasa kutokana na hofu iliyotanda kutokea Korea Kaskazini. Hii imekuja baada ya Korea Kaskazini kufanya jaribio lake la tisa la mabomu ya nyuklia.


31-05-2017; AFRISTEPHO BLOG

No comments

Powered by Blogger.
"