TUNAWEZAJE KUTUMIA ANTIBIOTIKI KUONGEZA UFANISI MWILINI MWETU










                                       ANTIBIOTIKI NI NINI?
antibiotiki ni dawa za kupambana na maambukizi kutokana na bakteria.hazisaidi zidi ya maabukizi ya virusi kama vile tetekuwanga,surua ya rubella,mafua au homa ya kawaida .ila kutokana na utendaji kazi aimanishi kila antibiotiki huweza kupambana na maambukizi ya bakteria.pia kitaalamu dawa za antibiotiki zenye muundo wa kikemikali unaofanana huchukuliwa kuwa katika familia moja. na ni muhimu kujua hilo kwa sababu 2.

             1.dawa za antibiotiki zinzo toka kwenye familia moja hutibu matatizo yanayo fanana.

             2.kama antibiotiki moja kutoka familia moja imeshindwa kuondoa matatizo basi inamaana na
                zengine kutoka familia hiyo hiyo azitoweza kufanya kazi hivyo utatakiwa kutumia antibiot
                iki kutoka familia nyingine.


                 UTARATIBU W MATUMIZI WA DOZI KIKAMILIFU




Dawa ya antibiotiki lazima itumike “kwa dozi kamilifu.” Kukatisha dozi bila kukamilisha siku zote za matibabu huweza kuyafanya maambukizi kuwa sugu zaidi.

Penisilini
Dawa kutoka familia ya penisilini ni miongoni mwa dawa muhimu zaidi katika kundi la antibiotiki. Penisilini hupambana na baadhi ya maambukizi, yakiwemo mengi ambayo husababisha usaha.

Penisilini hupimwa katika miligramu (mg) au uniti (U). Kwa penisilini G,miligramu 250 = 400,000 U.

Kwa watu wengi, penisilini ni miongoni mwa dawa salama zaidi. Kutumia zaidi ya dozi iliopendekezwa ni kupoteza fedha lakini huenda isimuathiri mtumiaji.

Usugu kwa dawa ya penisilini
Baadhi ya maambukizi yamejenga usugu dhidi ya penisilini. Hii inamaanisha kuwa zamani penisilini ilikuwa na uwezo wa kutibu mgonjwa mwenye maambukuzi haya, lakini kwa sasa haiwezi. Kama maambukizi hayatibiki na penisilini ya kawaida, antibiotiki nyingine inaweza kujaribiwa, au penisilini ya aina nyingine inaweza kusaidia. Kwa mfano, nimonia (kichomi) wakati mwingine huonesha usugu kwa penisilini. Tumia amoksilini badala yake.

Muhimu
Kwa ajili ya penisilini zote (ikiwemo ampisilini na amoksilini)

Baadhi ya watu wana mzio na penisilini. Mzio kiasi husababisha upele. Mara nyingi hujitokeza saa au siku kadhaa baada ya kutumia penisilini na hudumu kwa siku kadhaa.Ukitokea acha kutumia penisilini mara moja. Dawa za kupambana na mzio (Antihistamines) husaidia kupunguza muwasho. Tumbo kuvurugika na kuharisha kutokana na penisilini siyo dalili za mzio. Ingawa husababisha kero,zisiwe sababu za kusimamisha matumizi na dawa hiyo.

Kwa nadra sana, penisilini inaweza kusababisha mzio mkali sana-mlipuko wa mzio. Ndani ya dakika au saa kadhaa baada ya kutumia penisilini, mwili unaweza kututumuka,koo na midomo kuvimba, kupata tabu katika kupumua, hali ya kutaka kuzirai, na kuingia kwenye mshtuko. Hii ni hatari sana. Lazima achomwe sindano ya efedrini (adrenalin) mara moja. Wakati wote kuwa na epinefrini (epinephrine) tayari unapochoma sindano ya penisilini. Angalia Huduma ya kwanza.

Mtu yoyote ambaye amewahi kupatwa na mzio kutokana na penisilini kamwe asipewe – ampisilini, amoksilini, au aina za penisilini zingine tena,aidha kwa njia ya mdomo au sindano. Hii ni kwa sababu mzio unapotokea tena unaweza kuwa mbaya zaidi na hata kumuua. Watu wanaopata mzio kutokana na penisilini wanaweza kutumia erithromaisini au antibiotiki kama dawa mbadala.

Sindano
Penisilini mara nyingi hufanya kazi vizuri inapotolewa kwa njia ya mdomo. Sindano za penisilini zinaweza kuwa hatari. Zinaweza kusababisha mzio mkali na matatizo mengine. Tumia sindano za penisilini pale tu kunapokuwa na maambukizi makali au hatari.

Ampisilini na amoksilini
Ampisilini na amoksilini ni familia ya penisilini yenye tiba pana, maana yake ni kwamba huua aina nyingi za bakteria. Dawa hizi 2 mara nyingi ni mbadala wa nyingine.Pale ambapo ampisilini imependekezwa katika kitabu hiki, amoksilini inaweza kutumika katika nafasi yake kwa kuzingatia dozi sahihi.

Ampisilini na amoksilini ni dawa salama sana na ni msaada mkubwa kwa watoto wachanga na watoto wadogo. Ni muhimu sana katika kutibu maambukizi ya sikio. Ampisilini ni muhimu katika kutibu homa ya uti wa mgongo na maambukizi mengine makali miongoni mwa watoto wachanga. Amoksilini hutumika kwa ajili ya nimonia.

Madhara ya pembeni
Dawa hizi 2, lakini hasa ampisilini, huwa na tabia ya kusababisha kichefuch

      KIPI KIFANYIKE ZAIDI KIZIDI KUONGEZA UFANISI WA DAWA
1.hakikasha unapokea maelekezo ya kukamilika na kueleweka kutoka kwa mtaalamu wa tiba ili kuweza kuongeza ufanisi zaidi wa dawa
2.usipende kuacha dozi pasipo kupata ushauri wa mtaalamu hicho ni muhimu zaidi
3.usipende kumlazimisha mtaalamu akupe antibiotiki pasip kuonekana tatizo
4.usipende kuchukua antibiotiki ambyo imesha tumika na mtu mwingine ili kutibu tatizo
5.penda kumshirikisha mtaalamu juu ya ufanyaji kazi baadhi ya antiotiki ulizo wahi kutumia kipindi cha nyuma ili kuongeza ufanisi wa dozi.

je ni kweli matumizi ya antibiotiki kwa mdaa mrefu yaweza kuchangia usugu wa maabukizi?????

   jibu lake apo ni ''ndio'' matumizi ya antibiotiki kwa mda mrefu hutengeneza usugu mkubwa ndani ya mwili kitaalamu wanaita ''drug tolerance''ambapo hutokea maranyingi kutumia dawa kupita maelezo ambapo maambukizi huwa sugu juu ya utendaji wa dawa iyo kwa kujikinga na dawa iyo

No comments

Powered by Blogger.
"