KOREA KASKAZINI YAHUSISHWA NA UDUKUZI UNAOENDELEA HIVI SASA DUNIANI


Kumekuwa na sintofahamu juu ya hali na usalama wa matumizi ya mitandao kwenye maeneo mbali mbali duniani hivi sasa.
Hali hii imejengwa na udukuzi mkubwa unaoendelea kwa sasa duniani. Kirusi cha kuharibu mawasiliano na habari za mitandao kifahamikacho kama "Wannacry" kimevamia sehemu mbali mbali duniani nakufanya uharibifu pamoja na udukuzi wa habari nyeti za mitandaoni kwa makampuni mbalimbali duniani. Hadi hivi sasa bado jumuiya ya wanamitandao wana hali tete juu ya sakata hili
Taarifa zisizo rasmi zinalihusisha taifa la Korea Kaskazini juu ya uvamizi huu wa kimtandao ufahamikao kama "Cyber Attack". Hii Imetokana na taarifa ya mtafiti na mwana usalama wa mtandao wa Google Neel Mehta.
Mtafiti huyu pamoja na taarifa mbali mbali zinasema kirusi hiki cha "Wannacry" kina tabia na matendo yote yanayofanana na virusi vingine vilivyowahi kuharibu na kudukua taarifa mbali mbali za sony group mwaka 2014 na benki ya Bangladesh mwaka 2016 vilivyotengenezwa na kundi maarufu la udukuzi wa mitandao linalofahamika kama "Lazarous Group". Kundi hili linasemekana kuasisiwa na Korea Kaskazini na linafanya kazi na china chini ya udhamini wa Korea Kaskazini.
 Kundi hili ndilo lililofanya udukuzi mbali mbali duniani hasa ile ya mwaka 2014 ya kuvamia kampuni ya Sony.
Nchi zilizovamiwa na kirusi hiki hadi sasa ni pamoja na Marekani, Uingereza, Hispania, Urusi na Ufaransa.

Kirusi cha Wannacry kinashutumiwa na wanamitandao mbali mbali duniani kutokana na uharibifu mkubwa unaofanywa na kirusi hicho.

No comments

Powered by Blogger.
"