MWANDISHI WA HABARI NA MTANGAZAJI WA MADAWA YAKULEVYA AUWAWA
Aliyekuwa mtangazaji na mwandishi wa habari huko bara la Marekani ya kusini Javier Valdez ameuwawa na mtu asiyejulikana huko nchini Mexico.
Javier Valdez (50) aliechukua tuzo ya mwandishi na mtangazaji bora kuhusu madawa ya kulevya huko nchini Mexico na bara la Marekani ya Kusini mwaka 2011, alikutwa na mauti hayo baada yakumiminiwa risasi na mtu asiyejulikana huko Mexico.
valdez aliuwawa huko katika mji wa Culiacan ambapo alikuwa akifanya kazi katika shirika la RioDoce Website Reports.
Mwaka jana katika uzinduzi wa kitabu chake alikaririwa akisema "Kuwa mwandishi wa habari ni kuwa katika listi ya kifo, hata kama ukivaa nguo zakuzuia risasai, genge la wauza madawa wanaweza kuamua ni lini ama siku ipi waamue kukuua"
katika kipindi cha uhai wake alikuwa akiandika nakuripoti habari kuhusu madawa yakulevya kusini mwa bara la Marekani kwa miongo mitatu hasa uandishi na habari juu ya genge maarufu la madawa yakulevya nchini Mexico "Sinaloa Drug Cartel", ambalo lilijihusisha na uingizwaji wa madawa yakulevya nchini marekani kwa zaidi ya asilimia 25%.
Ikumbukwe Javier Valdez anakuwa mwandishi wa tano kuuwawa mwaka huu nchini Mexico.
16-MAY-2017,AFRISTEPHO BLOG
No comments