MASHOGA WAWILI KUCHAPWA VIBOKO HADHARANI


Mapenzi ya jinsia moja yamekuwa na kigugumizi katika jamii nyingi za kiafrika, huku yakipewa chapuo na kupigiwa debe na wanaharakati wa haki za kibinadamu duniani.
Hii imekuwa tofauti kwa nchi na jamii zingine duniani hasa zenye misimamo mikali ya kidini. Jambo hili limekuwani la kawaida kwa nchi za ulaya magharibi na marekani ila limekuwa kama dhahma na kosa la jinai kwa nchi nyingi za uarabuni na ulaya mashariki kutokana na changamoto nyingi wapenzi wa jinsia moja wanazokutana nazo.
Huko nchini Indonesia katika mji wa Aceh, mahakama ya "sharia" imehukumu wanaume wawili waliokuwa wanajihusisha na mapenzi ya jinsia moja kuchapwa viboko 85 kila mmoja hadharani nchini. Hukumu hiyo itafanyika hapo baadae nchini humo katika sherehe za kitaifa mnamo tarehe 23 mwezi huu katika mji wa Banda Aceh walipokutwa hatiani.
Vijana hao wenye umri wa miaka 20 na 23 walikutwa kitandani pamoja nakutiwa hatiani baada ya kuhojiwa na kukiri juu ya sakata hilo.
Suala la mapenzi ya jinsia moja si kosa katika nchi hiyo ila ni kosa na Marufuku katika mji wa Aceh, uliopo nchini humo.


Mahakama ilisema pia kuwa hii itakuwa fundisho na katazo kwa watu wengine wenye tabia hizo katika mji huo

MAY, 17-2017; AFRISTEHO BLOG

No comments

Powered by Blogger.
"