TRUMP-KUMFUKUZA KAZI MKUU WA SHIRIKA LA UPELELEZI KUMELETA UTULIVU
Zikiwa ni siku kadhaa tangu aliyekuwa mkuu wa shirika la upelelezi la Marekani "FBI" Mr. Comey atolewe madarakani na Raisi Donald Trump, amesema hali hiyo imeleta utulivu ndani na nje ya Marekani kutokana na vugu vugu na kelele za viongozi na baadhi ya maafisa kudai alisaidiwa na Urusi katika uchaguzi uliopita.
Ripoti za hivi karibuni zilimnukuu Raisi Donald Trump kabla ya kwenda kwenye ziara yake ya kwanza ya kiofisi tangu achaguliwe kuwa Raisi wa nchi hiyo nchini Saudia Arabia.
"Nilimfukuza kazi kwa kuwa hakuwa akiitendea haki nafasi yake, Nilipata presha kubwa juu ya suala hii sababu ya Urusi" alisema Trump kulingana na ripoti hiyo. Mr.Comey amesema atathibitisha yakuwa kulikuwa na muungano kati ya Trump na nchi ya Russia kabla ya kamati ya upepelezi iliyoundwa kuchunguza hilo.
Ikulu ya Marekani "White House" haijaweka wazi juu ya lugha iliyotumika katika mkutano wa Raisi trump na waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov pamoja na balozi wa Urusi nchini Marekani Sergei Kislyak
20-MAY; AFRISTEPHO BLOG


No comments