BAADA YA KIFO CHA PRINCE ROGERS, WARITHI WATANGAZWA
Mahakama yatangaza warithi wa mali na mirathi mingine ya aliyekuwa mwanamuziki mashuhuri duniani "Prince Rogers Nelson" tangu alipofariki mwaka 2016 mwezi Aprili. Dada wa mwanamuziki huyo na nduguze watano wametangazwa na mahakama kuwa warithi wa mali za mwanamuziki huyo.
Prince alifariki tarehe 21 mwezi Aprili mwaka 2016 akiwa na miaka 57 kwa kuzidisha dawa zakutuliza maumivu na msongo wa mawazo akiwa studion kwake. Ikumbukwe mwanamuziki huyu hakuwahi kuwa na mtoto. Ikiwa ni mwaka sasa umepita tangu kifo hicho kitokee mahakama imetoa haki kwa dada yake pamoja na nduguze kupewa mali za mwanamuziki huyo aliyekuwa na utajiri wa dola za kimarekani milioni 200. Ingawa utajiri huo utapungua kutokana na tozo ya kodi kutojumuishwa kwenye mali hizo.
Hii imekuja baada ya kijana mmoja aliyekuwa gerezani kudai alikuwa mtoto wa mwanamuziki huyo. Jaji wa mahakama aliamrisha apimwe DNA naku thibitika hakuwa mtoto wa mwanamuziki huyo na nduguze kupewa chapuo na haki juu ya mali hizo.
Ijapokuwa dada yake Tyra Nelson na nduguze john nelson, Omar Baker, Norrrine Nelson, Alfred jackson na Sharon Nelson kutangazwa kuwa warithi itawapasa kusubiri hadi mwaka mmoja ili kuweza kupatiwa mirathi hiyo.
Alizaliwa mwaka 1958, tarehe 7 mwezi wa 6. Alikuwa mwanamuziki, dansa, mwigizaji na mtunzi wa nyimbo mbali mbali duniani.
20-MAY; AFRISTEPHO BLOG


No comments