REKODI ZA JOSE MOURINHO MBELE YA ARSENE WENGER

Imekuwa hali ya kawaida kwa kocha wa Arsenal, Arsene Wenger kukwaruzana na hasimu wake mkubwa ambaye ni kocha wa manchester united kwa sasa Jose Mourinho.
Rekodi mbali mbali zimejengwa na mahasimu hawa wawili toka waanze kukutana katika michuano mbali mbali na mara nyingi arsenal imekuwa ikipata wakati mgumu kupata matokeo mbele ya Jose Mourinho.
Wakati Jose Mourinho akiwa kama kocha wa chelsea amekutana na  hasimu wake Arsene Wenger mara 15, na Arsenal imeweza kujinyakulia ushindi mara moja tu katika mechi hizo, na hiyo ilikuwa mwaka 2015 katika kombe la ngao ya hisani na hapo baadae arsenal ikakubali kichapo cha goli mbili kwa bila stamford bridge.
  • katika michuano ya ligi kuu ya uingereza Arsene wenger ameshindwa kupata ushindi hata mara moja na kuambulia sare mara 6 na Jose mourinho kushinda mara 5.
  • katika kombe la ligi(capital one cup), Arsene wenger hajawahi kushinda mechi yoyote mbele ya Mourinho kwa kukubali kufungwa mara zote mbili walizokutana.
  • Ngao ya hisani(community shield) wametoka sare kwa kila mmoja kushinda mbele ya mwenzake mara moja.
Jumla ya michuano yote waliyokutana Arsene wenger ameambulia ushindi mara 1 na kukubali kichapo mara zote 8 alizokutana na Jose mourinho. wameweza kutoka sare mara 6 tu.



Je, Arsene wenger anaweza kumaliza uteja huu akiwa anamkaribisha hasimu wake na kikosi kizima cha Manchester united ndani ya viunga vya emirates leo? Tusubiri tuone.


No comments

Powered by Blogger.
"