MAJAJI WAPIGIA CHAPUO MAPENZI YA JINSIA MOJA
Inawezekana ikawekwa historia katika bara la Asia kwanchi ya Taiwan kuwa taifa la kwanza kuruhusu ndoa za wapenzi wa jinsia moja.
Hii imekuja baada ya majaji wa mahakama kuu kuyapigia chapuo mahusiano hayo na kuweza kutengeneza mazingira mazuri kwa washiriki wa mapenzi ya jinsia moja kuruhusiwa hapo mbeleni. Hali hii imeleta mkanganyiko na sintofahamu kwa makundi mengine yanayokinzana na mapenzi ya jinsia moja nchini humo.
Hatua hii imefikiwa baada ya majaji wakuu kudai sheria juu ya mahusiano kwa sasa nchini humo haiwatendei haki wapenzi wa jinsia moja nchini humo na sharti kulitaka bunge nchini humo kupitia upya sheria hiyo ndani ya miaka miwili kuanzia sasa ama kutunga sheria mpya yenye kuwapa haki wapenzi wa jinsia moja.
Mahakama kuu nchini humo ilinukuliwa ikisema "kutoruhusu wapenzi wa jinsia moja kutofunga ndoa kwa minajili ya kulinda maadili na maudhui ya jamii, kunawanyima haki na usawa wapenzi hao".
24-MAY; 2017, AFRISTEPHO BLOG
No comments