AJAX KUFUA DAFU MBELE YA MACHESTER UNITED?
Zakiwa zimebaki dakika chache kuelekea fainali ya michuano ya "EUROPA LEAGUE" hii leo, klabu ya Ajax inatazamiwa kama inaweza kutunishia klabu ya Manchester United.
Fainali hiyo itakayopigwa Jijini Stockholm majira ya saa 3;45 usiku kwa saa za Afrika Mashariki. Akizungumza kabla ya mpambano huo kocha wa Manchester united Jose Mourinho alisema "tumejiandaa vema kwea ajili ya mchezo, hii ni kazi yetu na kilicho tuleta huku ni kazi na si vinginevyo, nina imani tutashinda kwa maana tumejiandaa vema kisaikolojoa na kimchezo". Aliongeza pia leo usiku beki wa Klabu hiyo Eric Bailly atakosekan kwa kuwa bado anaendelea kutumikia adhabu ya kadi nyekundu aliyoipata katika mchezo wa nusu fainali dhidi ya Celta Vigo.
vile vile ni faraja kwa wachezaji wa Manchester United na mashabiki wa Klabu hiyo baada ya beki Chris Smalling na Phil Jones kurudi kikosini.
Klabu ya Ajax inatazamiwa kutoa upinzani mkubwa kwa Mashetani hao wekundu wa jiji la Manchester katika mtanange huo.
24-MA- 2017; AFRISTEPHO BLOG
No comments