MOURINHO ANENA HAYA BAADA YA USHINDI


Zikiwa zimepita saa kadhaa tangu mtanange wa fainali ya "EUROPA LEAGUE" ambapo klabu ya soka ya nchini Uingereza manchester United kuibuka kidedea kwa ushindi wa goli 2 kwa bila. Mchezo huo uliopigwa jijini Stockholm uliweza kuwafanya mabingwa hao wapya wa kombe hilo kuweza kutumia dakika 48 tu za dakika zote 90 kujihakikishia ushindi wa kombe hilo.
Katika mchezo huo manchester United iliweza kujinyakulia ushindi wake kupitia kwa wachezaji wake mahiri Paul Pogba alieandika goli la kwanza na Henrikh Mkhitaryan aliefunga hesabu za ushindi katika dakika ya 48' nakuwafanya Machester united kuwa mabingwa wapya wa kombe hilo.
Baada ya mchezo huo Kocha wa Manchester united alisema "Nimefurahi kupata ushundi huu, ulikuwa msimu mgumu kwetu lakini tumemalizaa kwa kubeba kombe, hii ni njia bora katika timu kuliko kumaliza nafasi ya nne, tangu mwanzo wa msimu niliamini kwamba tutashinda taji hili na juhudi na bidii zetu zimetufanya tushinde taji hili. Ajax ni timu nzuri ila sisi tulikuwa bora kuliko wao, tumeumaliza msimu huu uliokuwa mgumu kwetu lakini kwa staili yaki tofauti kabisa kwa kunyakua kombe hili"
Kwa ushindi huu unafanya kocha Jose mourinho kubeba mataji yote katika ngazi za vilabu akiwa nyuma ya Georgio Trappatoni anyeongoza, na pia inaifanya klabu ya Manchester United kuwa klabu yenye makombe mengi nchini Uingereza kwa kubeba jumla ya mataji 45.






25-MAY-2017; AFRISTEPHO BLOG

No comments

Powered by Blogger.
"