JE, ATHLETICO MADRID WANAWEZA KUZUIA HILI LISITOKEE LEO?
Ikiwa leo ni muendelezo wa usiku wa Uefa ndani ya viunga vya "vicente Calderon", ambapo klabu ya Athletico Madrid itakuwa nyumbani kuwakaribisha vinara wa soka wa ligi kuu ya hispania Real Madrid katika mtanange wa pili wa michuano hiyo.
Katika mchezo wa kwanza uliopigwa "Santiago Bernabeu" Real Madrid waliweza kupata ushindi wa magoli 3-0 mbele ya mahasimu wao Athletico Madrid. Ushindi huu ulichagizwa na magoli yote matatu kufungwa na cristiano Ronaldo katika mechi hiyo.
Swali ni je, leo wataweza kumzuia Ronaldo asiwekee rekodi yake mbele yao? Ikumbukwe katika mechi ya kwanza ndani ya ligi kuu nchini humo Ronaldo aliweza kufunga magoli matatu(hat trick) mbele ya athletico madrid na pia kufanikiwa tena kufunga magoli hayo hayo matatu katika mashindano ya klabu bingwa barani ulaya.
Ronaldo amekuwa mchezaji wa kwanza kufunga magoli 10 katika misimu 6 mfululizo ndani ya michuani hiyo ya klabu bingwa barani ulaya. Ameweza kujinyakulia kiatu cha dhahabu katika michuano hiyo mara kadhaa huku akishikilia rekodi ya kuwa mfungaji bora wa muda wote wa michuano hiyo akiwa na magoli 106 mpaka sasa.
Kwa sasa Cristiano Ronaldo ana magoli 10 katika michuano hii huku akiwa anahitaji goli 1 tu kuwa sawa na mpinzani wake Lionnel Messi.
Amebakisha michezo miwili mkononi ambayo ni mchezo wa leo na fainali(kama wataweza kufuzu hivi leo) ili kuweza kumfikia na pengine kumzidi hasimu wake mkubwa Lionnel Messi.
JE, ATHLETICO MADRID WANAWEZA KUZUIA HILO LISITOKEE HIVI LEO KATIKA MCHEZO WAO?
MAY-10-2017, AFRISTEHO BLOG
No comments