HATIMAYE JUVENTUS YAWA TIMU YA KWANZA YAFUZU KUCHEZA FAINALI
Hatimaye klabu ya soka nchini Italia, Juventus imefanikiwa kufuzu kucheza fainali ya michuano ya UEFA champions League. Juventus inakuwa timu ya kwanza kwa mwaka huu kuweza kufuzu kucheza fainali hizo.
Hii ni kutokana na ushindi wa magoli 2-1 walioupata mbele ya timu ya AS Monaco. Wakiwa uwanja wao wa nyumbani Klabu ya Juventus iliweza kujipatia mabao hayo kupitia kwa Mario Mandzukic katika dakika ya 33' na bao la pili lilipachikwa na Dani Alves dakika ya 44'.Wakati bao la kufutia machozi la As Monaco liliweza kupachikwa na mchezaji Kylian Mbappe dakika ya 69'
Hii inakuwa ni mara ya pili kwa juventus kucheza fainali hizi ndani ya miaka mitatu tangu mwaka 2011 uanze. Ikumbukwe klabu ya Juventus katika fainali zamwaka 2015 dhidi ya Barcelona ilipoteza kwa kukubali kichapo cha mabao 3-1, na mwaka huu wameingia tena fainali. Ushindi huu umewafanya klabu ya Juventus kupata ushindi wa magoli 4-1 mbele ya Monaco baada ya mechi ya kwanza kuwafunga magoli 2 kwa bila.
MAY, 2017; AFRISTEPHO BLOG
No comments