HATIMAYE MADRID YAFANYA KWELI ULAYA


Usiku wa kuamkia leo kulikuwa na mtanage wa kukatana shoka kati ya wenyeji Athletico Madrid waliokuwa nyumbani kuwakaribisha vinara wa ligi kuu ya hispania Real Madrid.
Katika mchezo huo licha ya klabu ya Real Madrid kupoteza kwa kukubali kichapo cha goli 2 kwa moja, wamefanikiwa kuingia fainali ya michuano hiyo kwa mara ya pili ndani ya misimu miwili mfululizo.
Katika mchezo huo Athletico Madrid ndiowalioanza kupata magoli kupitia kwa Saul neguez katika dakika ya 12' alieunganisha vema mpira wa kona, na bao la pili liliwekwa kimiani na Antoine Greizmann katika dakika ya 16' kwa mkwaju wa penati.
Goli la kufutia machozi la Real Madrid lilifungwa kiungo Isco katika dakika ya 43' baada ya kazi nzuri ya Karim Benzema.
Kwa matokeo haya yanamfanya kocha wa sasa wa real madrid Zinedine Zidane kuweza kuingia fainali mara mbili ndani ya miaka miwili akiwa kama kocha wa klabu hiyo. Ikumbukwe kuwa msimu uliopita ndio ulikuwa msimu wake wa kwanza kama kocha ndani ya klabu hiyo nakufanikiwa kubeba taji hilo, na sasa amefanikiwa kuingia fainali hizo tena.
JE, JUVENTUS WATAWEZA KUZUIA REAL MADRID WALINYANYUE KOMBE HILO KWA MARA YA PILI MFULULIZO?







MAY,11- AFRISTEPHO BLOG

No comments

Powered by Blogger.
"