KENDRICK LAMAR AANGUKIA MIKONONI MWA POLISI
Siku ya jana ijumaa ya Mei 12, haikuwa nzuri kwa rapa wa Marekani Kendrick Lamar baada ya kukutwa hatiani kwa kosa la kutembea na gari lisilo na usajili wa namba.
Rapa huyo anayefanya vyema na single yake ya "HUMBLE" pamoja na albamu yake ya "DAMN" alisimamishwa na polisi katika maeneo ya Beverly Hills katika Mji wa Los Angeles huko marekani kwa kosa hilo.
Chombo cha habari cha Marekani "TMZ" kilimuona rapa huyo akiwa ndani ya gari yake Mercedes G-Wagon na punde tu baada ya rapa huyo kuona kamera zikimulika gari lake akapandisha vioo kuepuka kupigwa picha.
Polisi aliemuhoji rapa huyo alisema "hakuwa na leseni ya usajili wa gari, ila yuko poa". Kendrick aliweza kuondoka bila kuchajiwa chochote na polisi huyo baada ya maongezi kadhaa.
gud
ReplyDelete