HUYU NDIYO REFA ATAKAYECHEZESHA FAINALI
Dr. Felix Brych ni jina geni masikioni mwa wapenzi wa soka. Refa huyu ni mzaliwa wa ujerumani na amezaliwa Agosti-03-1975, mwenye umri wa miaka 41 kwa sasa.
Refa huyu ameteuliwa na shirikisho la soka barani Ulaya kuchezesha fainali ya Uefa kati ya Real madrid na Juventus.Ni refa wa shirikisho la soka duniani FIFA na pia ni mwanachama wa chama cha marefa barani ulaya (UEFA).
Refa huyu ni mwanasheria nje ya soka na ana shahada ya tatu ya udaktari (Uzamivu) katika masuala ya sheria aliyoipata kuiptia masuala ya soka. Refa huyu pia aliwahi kuchezesha mechi baina ya Chelsea na Barcelona, ambapo Chelsea waliibuka kidedea katika mtanange huo. Alianza kazi ya urefa katika ligi ya ujerumani mnamo mwaka 2004, na hapo baadae akatunukiwa beji ya FIFA mwaka 2007.
Mwaka 2014, mwezi Mei alichezesha fainali ya "EUROPA LEAGUE" kati ya Sevilla na Benfica, ambapo Sevilla waliibuka kidedea kwa ushindi wa mikwaju ya penalti.
Tarehe 12 mwezi huu aliteuliwa kuchezesha fainali za klabu bingwa barani ulaya kati ya Real Madrid watakaochuana na Juventus mjini Cardiff, Wales.
Atasaidiwa na marefa wasaidizi kama Mark Borsch, Stefan Lupp na msaidizi wa nne atakuwa refa kutoka Serbia Milorad Mazic
MAY, 13-2017; AFRISTEPHO BLOG



No comments