FORBES WATOA LISTI YA WASANII MATAJIRI AFRIKA KWA MWAKA 2017.
Ni siku chache tu zimepita Tangu jarida la Forbes kutoa listi ya wasanii wakiafrika wenye mkwanja mrefu kwa mwaka 2017.
Kama ilivyo kawaida kuna sura tumezoea kuziona katika listi ya wasanii matajiri Afrika, lakini listi hii mpya ndani ya jarida la forbes yameingia na pia yameonekana majina mengine mapya pengine hata hukuyatarajia kuwemoTakwimu hizi za Jarida hili zimetumia vigezo kama thamani ya mikataba ya matangazo ya msanii, Umaarufu, pesa anayochaji kwa show, mauzo ya muziki kupitia mitandao mbali mbali, uuangaliwaji wa video zake ndani ya youtube, kuandikwa na kuonekana mara kwa mara ktk magazeti, uwekezaji wa msanii, ushawishi katika jamii na mambo mengineyo.
Listi hiyo imejumuisha wasanii kama;
1. Akon
Huyu ni msanii mwenye mauzo zaidi ya milioni 35 ya albamu zake zote. Ameshinda tuzo mbali mbali ikiwemo kutajwazaidi ya mara tano katika tuzo za grammy, ana ngoma zaidi ya 45 zilizoingia katika "billboard 100 hit songs" . Huyu ndiye kinara kulingana na jarida la forbes.
2. Black Coffee
Amejipatia umaarufu mkubwa sana barani Afrika hasa mwaka jana baada ya kushinda tuzo ya BET awards kule marekani. Black coffee ni jina la kisanii ila jina lake halisi ni Nkosinathi maphumulo aliyezaliwa katika jiji la muziki la Kwa Zulu Natal na baadae kukulia katika mji wa mashariki mwa South Africa kabla yakurudi tena Kwa Zulu Natal,
3. Hugh Masekela
Huyu ni mzaliwa waWitbank huko South Africa. Ameachia albamu zaidi ya 43 ambazo zingine zimewahi kuchezwa na Marvin Gaye, Paul simon, StevieWonder, Miriam Makeba na wengine wengi.
4. Don Jazzy
Huyu anatajwa kama msanii wa nne kwa utajiri Afrika na wa kwanza kwa Nigeria. Alianza kuimba kanisani kabla ya baadae kwenda nchini Uingereza kusomea muziki. Don Jazzy ni jina lake la stejini Lakini jina lake halisi ni Michael Collins Ajereh.
5. Tinashe
Huyu ni mzimbabwe mwenye uraia wamarekani. Alianza masuala ya "model" akiwa na miaka mitatu. Pia msanii huyu aliwahi kuonekana katika filamu ya mwaka 2000 iliyokuwa inajulikana kama "cora unshamed". Na pia sauti yake ilitumika katika filamu ya katuni iliyoitwa "Polar Express" sambamba na mshindi wa tuzo ya Oscar ya muigizaji bora Tom Hanks.
6. Jidenna
Anashika nafasi ya sita katika jarida la forbes kwa mwaka 2017. Msanii huyu mwenye asili ya nigeria akiwa na umri wa miaka 10 alikuwa anataka kuwa mwanamuziki lakini aliogopa kumwambia baba ake kwa kuwa baba ake alitaka awe engineer. Jina lake kamili ni Jidenna Theodore Mobisson.
7. Wizkid
Hivi sasa anafahamika kama mfalme wa muziki wa africa "King of African Music". Msanii wa marekani na mshindi wa tuzo za Grammy Alicia Keys na mumewe Swizz Beatz waliwahi kupost baadhi ya nyimbo za msanii huyu katika mtandao wa Instagram. Alicia keys alipost na kwenda mbali zaidi kwa kusema "This song makes me Happy". Kylie Jenner( mpenzi wa Tyga) aliwahi pia kupost katika mtandao wa Snapchat akiucheza wimbo wa Wizkid.
8. Davido
Huyu ni msanii mwingine kutoka Nigeria ambaye anashika nafasi ya 8 kulingana na Jarida la Forbes. Amefanikiwa kuutengeneza umaarufu wake ndani na nje ya Afrika kwa muda wa miaka mitano tu. Aliwahi kukaririwa pia akisema wasanii kama D'banj na P'square walimfanya hivi alivo sasa kuwa kinawezekana. Moja ya albamu iliyompa umaarufu mkubwa Davido ni albamu yake ya mwaka 2012 iliyotambulika kama "Omo Baba Olowo".
9. Sarkodie
Michael Owusu Addo, ndio jina halisi la msanii huyu, Ni msanii wa kwanza kutoka Ghana kushinda tuzo ya BET awards. Alianza kurap toka akiwa mdogo ana ameweza kujijenga na kuwa msanii mkubwa kupitia kwa aliekuwa meneja wake Duncan Williams. Ameweza kujijengea uhalisia wa aina yake katika muziki nje na ndani ya Afrika kupitia staili yake yakurap kwa mchanganyiko wa lugha zakiasili kutoka Ghana. Aliweza pia kuuza copy zaidi ya 4,000 katika siku ya kwanza alipoachia albamu yake ya kwanza nchini Ghana.
Ni mmoja kati ya waasisi wa staili ya kucheza muziki iitwayo "Azonto" ambayo asili yake ni kutoka katika dansi ya muziki wa asili iitwayo "Kpanlogo".
10. Oliver Mtukudzi
Huyu ndiye anafunga listi hii ya wasanii kumi matajiri kulingana na jarida la forbes kwa mwaka 2017. Ana albamu 65 kibindoni zaidi ya aliyekuwa mfalme wa Pop ulimwenguni marehemu Michael Jackson na Whitney houston. Amedumu kwa zaidi ya miaka 41 katika muziki na kutengeneza nyimbo ambazo zinaishi hadi leo. Forbes wamemtaja kama msanii wa 10 kwa utajiri afrika.
BONUS INFO
Afrika Mashariki haijaingiza msanii hata mmoja ndani ya listi hii kwa mwaka 2017 kulingana na jarida la Forbes. Hii ni idadi ya wasanii kwa kila nchi barani afrika.
1. Nigeria-4
2. Sengal-1 (Akon)
3. South Africa-2
4. Ghana-1
5. Zimbabwe -2
No comments