QATAR YAZIDI KUWA NA NGUMU KISIASA


Vikwazo na Marufuku vyazidi kuongezeka kwa nchi ya Qatar ya nchi mbali mbali kutuhumu ushirikiano wa nchi hiyo na genge la magaidi. Nchi majirani wa Qatar wanaituhumu nchi hiyo kuwa na ushirikiano na magaidi na zaidi pia kuwapa misaada mbali mbali magaidi hao.
Tayari nchi ya Misri inakaribia kufunga anga yake kwa ndege za Qatar kuweza kupita na pia hivi leo jumanne nchi za Bahrain na Saudia Arabia zinatarajia kufanya hivyo kama Misri. Qatar imekuwa ikituhumiwa kusaidia magaidi katika ghuba hiyo barani Asia.
Mara Kadhaa Qatar imekataa kuhusika na tuhuma hizo toka kwa nchi jirani, na tayari mabalozi wake katika nchi ya Saudia Arabia, Misri, Bahrain na UAE wameambiwa waondoke katika nchi hizo. Hiii Imeleta athari kwa makampuni ya ndege yanafanya kazi na nchi ya Qatar kama Emirates, Etihad na Qatar yenyewe.

06-06-2017; AFRISTEPHO BLOG

No comments

Powered by Blogger.
"