AJALI YA BASI LA WANAFUNZI MKOANI ARUSHA IMEONGOZA KWA WINGI WA VIFO BAADA YA HII
Ikiwa ni siku chache tangu vifo vya wanafunzi na walimu takribani 35 itokee mkoani. Leo hii wanachi wa mkoani Arusha na viongozi wa serikali walijumuika kwa pamoja pale mkoani Arusha kuaga miili ya wanafunzi wa shule ya Lucky Vicent waliofariki kwa ajali.
Ajali hii imeacha simanzi na majonzi makubwa kwa jamii nyingi ya watanzania pamoja na wanafamilia waliopatwa na msiba huo. Ukubwa wa ajali hii imechangiwa na uchache wa waliopona katika ajali hiyo.
Mnamo Aprili 21 mwaka huu (2017) nchini South Africa palitokea ajali nyingine kubwa iliyosababisha vifo vya wanafunzi takribani 20 waliofariki baada ya basi walilokuwa wanasafiria kugongana na lori katika barabara ya eneo la bronkhorstspruit na Verena katika mji mkuu wa south Africa, Pretoria. Ajali hii ilitokea kilometa 70 kutoka mji mkuu wa South africa, Pretoria.
Mwenyezi Mungu azilaze Roho za watoto hawa mahala pema peponi
MEI-09-2017, AFRISTEPHO BLOG
No comments